Uongozi wa mkoa Katavi umesema hautabomoa vibanda vya Wafanyabiashara (Wamachinga) bila kuwashirikisha Wafanyabishara hao.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametangaza hatua hiyo katika kikao cha kujadili namna ya kuwapanga Wafanyabiashara wadogo katika maeneĆ² mbalimbali ya kufanyia biashara.
Pamoja na kutoa tangazo hilo, Mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amewataka Wafanyabiashara hao kuheshimu sheria zilizopo ili wafanye biashara zao bila bughudha.
Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Katavi zinaonesha kuwa, kwa sasa kuna wafanyabiashara wadogo zaidi ya elfu 11 mkoani humo.