Biashara United yalamba milioni 10

0
117

Mkuu wa mkoa wa Mara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa timu ya mpira wa miguu ya Biashara United ya mkoani humo Ally Hapi amekabidhi shilingi milioni 10 kwa timu hiyo, ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa endapo itatoka sare katika mchezo wake dhidi ya timu ya Simba.

Kabla ya mechi hiyo Hapi aliahidi kutoa shilingi milioni 10 endapo timu hiyo ya Biashara United ya Mara itapata sare na shilingi milioni 15 kama itashinda katika mchezo huo na Wekundu wa Msimbazi.

Akikabidhi fedha hizo, Hapi amesema lengo ka kufanya hivyo ni kuhakikisha timu hiyo inapata ari na nguvu ya kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu na shirikisho la vilabu Barani Afrika.

Katika mchezo wake na timu ya Simba uliopigwa kwenye dimba la Karume mjini Musoma mkoani Mara tarehe 28 mwezi huu Biashara United ilitoka sare ya bila ya kufungana.