Chui auawa baada ya kujeruhi wanne

0
265

Watu wanne wamejeruhiwa na chui wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya chui huyo kuvamia zahanati ya Huruma iliyopo wilayani humo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema chui huyo anayedaiwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, alionekana majira ya asubuhi katika eneo la Bomang’ombe.

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni  Emmanuel Usara,  Jesca Nnko, Urusula Cosmas na Maliki Sakia wote wakazi wa Bomang’ombe wilayani Hai.

Hata hivyo askari kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) walifanikiwa kumdhibiti na baadaye kumuua chui huyo kabla hajaleta madhara zaidi.