Korea Kusini kusitisha ulaji wa mbwa

0
143

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in anaangalia ikiwa sasa ni muda sahihi wa kupiga marufuku ulaji wa mbwa nchini humo.

Rais Moon ambaye anapenda na anafuga mbwa, amesema anafikiria kupiga marufuku ulaji wa mbwa ikiwa ni moja ya njia mpya za kulinda wanyama waliotelekezwa.

Inasemekana kwamba ulaji wa nyama ya mbwa umeshuka ingawa bado takribani mbwa milioni moja wanachinjwa kwa mwaka.

Nchi ya Korea Kusini tayari imepiga marufuku uchinjani wa kikatili wa mbwa na paka ilaulaji wa nyama hizo haukuwahi kupigwa marufuku.