Mwanamuziki wa Marekani Robert Sylvester Kelly maarufu kwa jina la R Kelly amepatikana na hatia katika mashtaka yote yanayomkabili ikiwemo unyanyasi wa kingono kwa Wanawake na Watoto, rushwa, utekaji nyara na biashara ya ngono.
Katika kesi hiyo R Kelly anadaiwa kutumia umaarufu wake na utajiri wake kuwarubuni wanawake kwa ahadi za kusaidia kazi zao za muziki, baadhi ya Mashuhuda (Waathirika) wameiambia Mahakama kwamba walikuwa chini ya umri wakati wakinyanyaswa kijinsia.
Hukumu ya R Kelly inatarajiwa kutolewa May 04,2022 na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au kifungo cha maisha gerezani .