Rais Samia ateua watatu Tume ya Uchaguzi

0
350

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wajumbe watatu kujaza nafasi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kama ifuatavyo:

Kwanza, amemteua Asina Abdillah Omar ambaye ameteuliwa kwa kipindi cha pili kuendelea na majukumu ya tume baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika Septemba 15, 2021.

Pili, amemteua Magdalena Rwebangira kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na tatu, amemteua Jaji Jacob Mwambengele, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza Septemba 14 mwaka huu.