Likizo za Waganga wakuu wa wilaya zasitishwa

0
153

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesitisha likizo za Waganga wakuu wa wilaya mkoani humo, ili warudi kazini kuhamasisha utoaji wa chanjo ya UVIKO – 19.

Homera ametangaza uamuzi huo wakati wa semina iliyoshirikisha Wajumbe wa kamati ya afya ya msingi ya mkoa wa Mbeya.

Amesema amefikia uamuzi huo baada ya kuona zoezi la utoaji chanjo dhidi ya UVIKO – 19 mkoani humo si la kuridhisha.