Polisi wakamata meno ya tembo

0
146

Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa Rufiji linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na vipande 16 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 25.
 
Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Rufiji, Protas Mutayoba amesema watu hao wamekamatwa katika eneo la Utenge Kisevule wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
 
Thamani halisi ya vipande hivyo vya meno ya tembo bado haijajulikana.