Malima atoa maagizo bandari ya Tanga

0
170

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Adam Malima ameuagiza uongozi wa bandari ya Tanga kukutana na Wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo, ili kupitia upya tozo za usafirishaji wa mizigo.

Malima ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea bandarini hapo, kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa kila siku.

“Ni vizuri sasa mkakaa na Wadau pamoja na Wafanyabiashara ili mpitie upya gharama za usafirishaji kwenye bandari yetu, sisi tunataka kuwa washindani wa bandari ya jirani zetu hapo Mombasa na hili linawezekana.”ameagiza Malima

Amesema kitengo cha biashara katika bandari ya Tanga kina nafasi kubwa ya kufanikisha jambo hilo, na lengo kubwa ni kuhakikisha wanavutia watumiaji wengi zaidi katika bandari hiyo.

Miongoni mwa bidhaa muhimu zinazosafirishwa kupitia bandari ya Tanga ni Mkonge, ambao unasafirishwa kwenda nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Nigeria, China, Ghana na Ivory Coast.