Kesi ya kina Mbowe yakwama saa 3

0
136

Ushahidi wa kesi ndogo ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na wenzake watatu umeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Mokosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, baada ya kukwama kwa takribani saa 3 hii leo.

Kesi hiyo ilikwama kutokana na watu kutoruhusiwa kuingia na simu ndani ya mahakama, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuwepo kwa usambazaji wa habari zisizo rasmi mtandaoni wakati kesi ikiwa inaendelea.