Tanzania na China kushirikiana kuzalisha dawa za tiba asili

0
142

Waziri wa afya Dkt.Doroth Gwajima amesema Serikali imekusudia kuishirikisha Serikali ya China katika uwekezaji wa dawa asili na tiba mbadala ambapo tayari ekari 100 zimetengwa wilayani Kisarawe mkoani Pwani ili kufanikisha lengo hilo.

Katika hafla ya utiaji saini mkataba namba 26 wa madaktari kutoka China watakaotoa matibabu kwenye hospitali tofauti hasa za Kanda na mikoa nchini,Waziri Gwajima amesema China imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta ya Afya ikiwamo dawa asili . Pause Waziri Dorothy Gwajima

Hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Tasisi ya tiba ya mifupa na akili Muhimbili MOI, ambapo Balozi wa China Xu Chen amesema ushirikiano baina ya nchi hizo ni wa kihistoria hivyo China inafurahi kusaidia Tanzania katika kuboresha huduma mbaalimbali ikiwamo za afya nchini.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa MOI Respicious Boniface amesema mkataba huo una manufaa kwenye huduma za afya hususani upasuaji kwa kuwa richa ya wananchi kutibiwa pia madaktari kadhaa wazawa wanapata nafasi ya kujifunza zaidi hasa kwenye upasuaji ambapo Kuna uhaba wa wataalam changamoto

Ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na China katika kuboresha huduma za afya chini imedumu kwa zaidi ya miaka 50 huku miundombinu, vifaa tiba na utabibu zikiendele kuimarika zaidi mpaka hivi sasa.