Mwenge wa Uhuru wakagua mfumo wa kuhifadhi taarifa za wagonjwa

0
128

Kiongozi wa mbio maalum za mwenge Kitaifa 2021 Luteni Josephine Mwambashi akiangalia mfumo wa GoT-HOMIS katika kituo Cha afya Cha Mapogoro kabla ya mwenge kuweka jiwe la msingi la mradi huo wa mfumo wa Tehama unaofanya kazi kwa ajili ya ufuatiliaji malipo na taarifa za mgonjwa anaekwenda pata matibabu.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo hicho kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Josephine Mwambashi amesema utasaidia katika kuongeza Pato la Serikali na kuboresha huduma kwa wateja wanafika kupewa huduma

Akizungumzia mfumo huo, Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mapogoro wilaya ya mbarali dakta Wilbroad Ngoya amesema faida zilizopatikana tangua kuanza kwa mfumo huo Ni pamoja na utunzaji wa kumbukumbu za wateja na wagonjwa wanaopatiwa huduma kuimarika na taarifa zote kutumwa kwenye mfumo

Dkt. Ngoya amesema makusanyo ya miezi mitatu kabla ya kufunga mfumo yalikuwa wastani wa shilingi milioni Mia tatu sitini na nne,Mia sita therathini na tatu kwa mwezi na baada ya kufunga mfumo makusanyo yameongezeka Hadi kufikia wastani wa shilingi million 848,455 kwa mwezi