Jitihada zafanyika kunusuru samaki Mtera

0
6368

Mkuu wa wilaya.ya Iringa Mohamed Moyo amesema atakutana na wakuu wenzake wa wilaya za Mpwapwa na Chamwino mkoani mkoani Dodoma zinazopakana na Bwawa la Mtera, ili kukubaliana.kusitisha shughuli za uvuvi kwa miezi miwili kupisha uzalishaji wa samaki.

Uamuzi huo wa mkuu huyo wa wilaya ya Iringa unatokana na kupungua kwa samaki.kwenye bwawa hilo la Mtera kunakoelezwa kusababishwa na uvuvi.haramu.

Katika kukabiliana na uvuvi haramu kwenye bwawa hilo la Mtera, nyavu zipatazo 80 zilizo.chini ya.kiwango zenye thamani ya shilingi milioni 13 zimeteketezwa.na.moto, na watuhumiwa 12 kuchukuliwa hatua kwa kulipa.faini na kufikishwa mahakamni