Bilioni 50 zatolewa kununua mahindi

0
5870

Serikali imetoa shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kununua mahindi kutoka kwa Wakulima wa maeneo mbalimbali nchini.

Akiahirisha mkutano wa nne wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ununuzi wa mahindi hayo utaanza Jumatatu tarehe 13 mwezi huu.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema fedha hizo zitatolewa kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), ambao umekuwa ukifanya kazi hiyo ya kununua mahindi ya Wakulima.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha baada ya kusikia kilio cha Wakulima wa maeneo mblimbali nchini kuwa mahindi yao yamekosa soko.

Bunge limeahirishwa hadi tarehe 2 Novemba mwaka huu.