Tanzania mwenyeji onesho la utalii EAC

0
128

Tanzania itakuwa mwenyeji wa kwanza wa onesho la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EARTE), litakalofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 9 hadi 16 mwezi Oktoba mwaka huu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, lengo la onesho hilo kufanyika hapa nchini ni kuvutia na kukuza uwekezaji katika sekta ya utalii.

Amesema onesho hilo litakuwa linafanyika kwa mzunguko katika nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kila mwaka .

Onesho hilo litajumuisha siku tatu za maonesho na siku tano za ziara maalum ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na fursa za utalii wa ndani kwa Tanzania Bara na Zanzibar,.