Makalla awaonya madalali wanaopangisha nyumba Magomeni Kota

0
141

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amezihakikishia Kaya zote 644 wakazi wa Magomeni Kota kuwa   Serikali itawapatia Makazi watu wote wanaostahili na walioainishwa tokea awali ambapo amewataka kuwapuuza wote wanaosambaza taarifa za uvumi.

RC Makalla amesema hayo wakati alipofanya ziara ya Kujiridhisha na kukagua maendeleo ya Mradi huo Wenye thamani ya Shilingi bilioni 52.1 ambapo kwa Sasa Ujenzi umefikia 99% na ukikamilika utanufaisha Watu zaidi ya 3,000 kutoka Kaya 644 na sasa TANESCO wapo kwenye hatua za kuweka miundombinu ya umeme.

Aidha Makalla amesema Mradi utakapokamilika Wakazi husika wataitwa na kutangaziwa tarehe rasmi ya kuingia Katika nyumba hizo hivyo wawe watulivu.

Hata hivyo Makalla ametoa wito kwa Wakala wa Majengo TBA kutumia eneo lililobaki kimkakati kwa kujenga Majengo ya Gorofa ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Ardhi.

Pamoja na hayo Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi yake ya kusimamia na kukamilisha miradi yote ya maendeleo na hii inajirihidhisha kupitia Mradi wa Magomeni Kota.

Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi ya waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota ulianza October mosi 2016 ukihusisha Ujenzi wa Majengo matano yenye Gorofa nane Hadi Tisa ambapo ukikamilika wanufaika wataishi Bure ndani ya Nyumba hizo kwa kipindi Cha miaka mitano.