Ajali yaua watano, mmoja ajeruhiwa

0
175

 
Watu watano wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la King’ori wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso.
 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea katika barabara ya Arusha – Moshi, na kuhusisha gari lenye namba za usajili T 111 CUU aina ya Mitsubishi Fuso  pamoja na Mitsubishi Canter lenye namba za usajili T 612 BNN.

Kamanda Masejo amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
 
Amemtaja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Heriel Lyimo ambaye amelazwa katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro,  na kuongeza kuwa miili ya watu hao imehifadhiwa kwenye hospitali ya rufaa ya Mount Meru jijini Arusha.