Zaidi ya watu arobaini wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa, baada ya moto kuzuka katika gereza moja kwenye jimbo la Banten magharibi mwa Indonesia.
Moto huo ambao umezuka leo alfajiri umeteketeza maeneo kadhaa ya jengo la gereza la Tangerang, ambapo baadaye ulizimwa.
Jengo hilo la gereza limekuwa likihifadhi wafungwa ambao wanatumikia vifungo mbalimbali, kutokana na makosa yanayoambatana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
Jengo hilo ambalo lina uwezo wa kuchukua wafungwa 38 limekuwa likichukua wafungwa zaidi ya mara tatu ya uwemo wake, hivyo kusababisha msongamano wa wafungwa.
Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu nchini Indonesia imekiri kuwepo kwa msongamano wa wafungwa katika jengo hilo.
Uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha moto huo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.