Taifa Stars yaichapa Madagascar 3-2

0
2547

Timu ya Taifa (Taifa Stars) imeibuka kededea katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya timu ya Madagascar Katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mkapa mkoani Dar es Salaam.

Mchezo ulioanza majira ya saa 10:00 jioni Taifa Stars walikuwa wa kwanza kuliona lango la Madagascar baada Erasto Nyoni kufunga goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 2 ya mchezo huku
Novatus Dismas akishindilia bao la pili dakika ya 26 za kipindi cha kwanza.

Madagascar waliendelea kujiuliza kilichowapata walijipamga na kupitia Njiva Rakotoharimalala walipata goli la kwanza dakika ya 36, na dakika za nyongeza kipindi cha kwanza wakaongeza bao la pili na timu zote kwenda mapumziko zikitoshana magoli 2-2

Kila timu zilirudi uwanjani baada ya mapumziko na maelekezo ya makocha na kwa Taifa Stars wakajipatia goli la tatu Katika dakika ya 53 Feisal Salum Toto akaongeza bao la ushindi na mwisho kwa Taifa Stars

Taifa Stars ipo kileleni kwa kundi
Kundi J ikiwa na Alama 4 ikifuatiwa na Benin yenye Alama 4 wakati Congo DR wakiwa nafasi ya 3 kwa Alama 2 mkia ukiburuzwa na Madagascar wakiwa hawana alama yoyote.