Waziri Bashungwa aipongeza Stars

0
2511

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars na Watanzania wote kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Timu ya Madagascar kwenye mchezo uliochezwa leo Septemba 07, 2021 wa michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Bashungwa ameeleza kuwa wizara itawapa zawadi ya shilingi milioni 10 kuwapongeza kwa jitihada safi waliyoonesha.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa kuwaomba wadau mwenye zawadi kwa Taifa Stars wawasiliane na wizara ili kutambua zawadi ya michango hiyo ya hamasa kwa timu hiyo.