Wadau wa mazingira wakutana

0
109

Wadau wa mkutano wa kikanda wa mazingira kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Paris ya utunzaji wa mazingira, wanakutana mkoani Morogoro kujadili masuala mbalimbali.

Mkutano huo wa siku tatu unafanyika kwenye kituo cha kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Wadau kutoka nchi nne ambazo ni Tanzania, Botswana, Kenya na Gambia wanashiriki katika mkutano huo.

Mkutano.huo wa kikanda wa mazingira unafanyika kwa njia ya mtandao, ambapo kwa upande wa Tanzania wadau wanashiriki wakiwa kwenye kituo hicho cha Kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa

Wakati wa mkutano wao, Wadau hao pia watajadili kilimo cha utomvu, matumizi yake na namna kilimo hicho kinavyoweza kutumika katika utunzaji wa mazingira.