Taifa Stars yaahidi kuinyuka Madagascar

0
2457

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Paulsen amesema kikosi Cha timu hiyo kipo imara tayari kuikabili timu ya Taifa ya Madagascar kwenye mchezo wa kuelekea kufuzu fainali za kombe la Dunia

Paulsen amesema hayo leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam sikumoja kabla ya mchezo huo.

Kwa upande wake Nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Erasto Nyoni amesema kuwa wapo tayari kuibuka na ushindi kwani wana ari kubwa ya ushindi ili kujiweka nafasi nzuri kwa michezo itakayofuata

“Tunashukuru wachezaji wote tupo vizuri na matarajio yetu ni kupata pointi tatu muhimu kwa mechi zote 3 tutakazocheza hapa nyumbani.”

Aidha, Ofisa Habari na Mawasiliano TFF, Cliford Ndimbo amesema mchezo huo utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10:00 jioni hautahusisha mashabiki uwanjani kutokana na maelekezo ya FIFA ili kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19.