Waliopindua serikali Guinea watoa amri kwa mawaziri

Mapinduzi

0
324

Wanajeshi waliopindua serikali ya Guinea Septemba 5, 2021 wameamuru mawaziri wa serikali na viongozi wa kitaifa wote kuhudhuria mkutano baadaye leo, na kwamba yeyote ambaye hatahudhuria atachukuliwa kama mwasi.

Katika matangazo kwa umma kupitia runinga wamesema makamanda wa kijeshi wamechukua nafasi zote za wakuu wa mikoa na kwamba Rais aliyepinduliwa, Alpha Conde yupo salama lakini akiwa kizuizini, huku amri ya kutokutembea usiku ikitolewa.

Mapinduzi hayo yamelaaniwa na Umoja Wa Mataifa na Umoja Wa Afrika.

Kiongozi mkuu wa vikosi maalumu vya jeshi, Kanali Mamady Doumbouya amesema amelazimika kuchukua madaraka kwa sababu anataka kumaliza matatizo ya rushwa yaliyokithiri na uongozi mbaya.