Serikali yajipanga kukabiliana na uchafu wa mazingira

0
139

Serikali mkoani Mara imeanza kampeni ya usafi wa mazingira ili kuuweka mkoa huo safi na wenye kuvutia.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa huo, Ally Happi amesema Serikali imebaini uwepo wa maeneo mengi machafu hasa sehemu za mikusanyiko hivyo ni vema kuanza kupambana na hali hiyo ili kuleta mandhari zuri na safi kwa mkoa huo.

Amesema kwa kuanza watahakikisha kila mtu katika eneo la nyumba yake au biashara anafanya usafi ikiwemo kusafisha mitaro na kuondoa taka ngumu.

Hapi amesema ili kuleta ufanisi katika kampeni hiyo, wanatarajia kuzishindanisha halmashauri zote za mkoa huo jambo ambalo litaleta chachu na hali ya kujituma zaidi.

Amesema usafi wa mazingira ni tiba kwa magonjwa mbalimbali kama vile kuhara, kichocho, kipindupindu na malaria.

Hapi amewataka watumishi wa sekta ya afya kusimamia zoezi hilo kwa weledi kwani wao ndo kikwazo kutokana na kutokutilia maanani usafi wa mazingira.

Ameongeza kuwa Watumishi wengi wa sekta ya afya wamekuwa wakipambana na masuala ya mama lishe huku wakipuuza kusimamia usafi wa mazingira.

Mkoa wa mara unajipanga kufanya kampeni mbalimbali za kijamii zikiwemo zile za uchumi, biashara, kilimo na upandaji miti.