Hamza alikuwa gaidi : DCI

0
146

Jeshi la Polisi nchini limekamilisha uchunguzi wa awali wa tukio la kuuawa kwa watu wanne wakiwemo askari wake watatu lililotokea  hivi karibuni mkoani Dar es Salaam, na kudai kuwa uchunguzi huo umethibitisha mhusika wa tukio hilo alikuwa ni gaidi.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Camilius Wambura amewaeleza waandishi wa habari jijini Mwanza kuwa, mtuhumiwa wa tukio hilo Hamza Mohamed alikuwa ni gaidi aliyedhamiria kuleta madhara makubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

Amesema tukio lilitotokea Agosti 25 mwaka huu katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Ali Hassan Mwiny lilikua ni la kigadi, na Hamza alikuwa ni gaidi wa kujitoa muhanga.