Fedha za tozo kujenga madarasa

Tozo na Maendeleo

0
152

Rais Samia Suluhu Hassan amesema fedha zitakazokusanywa katika tozo za miamala ya simu mwezi huu wa Septemba na Oktoba mwaka huu, zitatumika kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya 500 nchini na kuboresha miundombinu ya elimu.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Tegeta mkoani Dar es Salaam aliposalimiana na Wakazi wa eneo hilo, akiwa njiani kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani kurekodi filamu yenye lengo la kuitangaza Tanzania.

Amesema hatua hiyo itawawezesha Wanafunzi wanaotaka kuanza shule au kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2022 kukuta vyumba vya madarasa viko tayari pamoja na miundombinu mingine ikiwa imeboreshwa.

Rais Samia Suluhu Hassan amewaeleza Wakazi hao wa Tegeta na Watanzania wote kuwa tozo zitaendelea kuwepo, kwa sababu zinasaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amefafanua kuwa, katika kipindi cha miezi miwili pekee tangu Serikali ilipoanza kutoza tozo katika miamala ya simu imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 60, ambazo zitatumika kujenga vituo vya afya 220 katika maeneo mbalimbali nchini