Bei ya mafuta kupanda

0
116

Bei ya mafuta itapanda kuanzia hapo kesho kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dodoma na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), katika bandari ya Dar es Salaam bei ya petroli imeongezeka kwa shilingi 84, dizeli shilingi 29 na mafuta ya taa bei imeongezeka kwa shilingi 18.

Katika bandari ya Tanga bei ya petroli imeongezeka kwa shilingi 53, dizeli shilingi 14 na ya mafuta ya taa itabaki kama ilivyokuwa.

EWURA imesema katika bandari ya Mtwara petroli imeongezeka shilingi 108 na dizeli shilingi 46,

Taarifa hiyo ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji imesema bei ya mafuta katika mikoa mingine itategemea na wanachukulia wapi mafuta hayo kati ya bandari hizo, lakini bei ni elekezi.