UWT Mwanza wapigwa jeki

0
196

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mary Masanja amekabidhi kompyuta 2, mitungi ya gesi ya kupikia 100 na kuwawezesha kinamama wa Jumuiya za UWT Wilaya ya Ilemela na Nyamagana kuanzisha miradi midogo midogo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Naibu waziri huyo ametoa pia msaada wa pikipiki kwa UWT katika wilaya hizo

Akikabidhi vitu hovyo Naibu waziri Masanja amesema pikipiki alizotoa zitasaidia kufanya shughuli ndogo ndogo ili wapate fedha zitakazoongeza mapato ya jumuiya hizo na kompyuta itasaidia katika uendeshaji wa shughuli za ofisi.

Akikabidhi majiko ya gesi ya kupikia Masanja amesema lengo ni kuwahimiza kinamama kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti hovyo na kuacha matumizi ya kuni na mkaa.

Naibu waziri huyo amezihimiza jumuiya hizo kuanzisha miradi ya ufugaji nyuki itakayowawezesha kuvuna asali ambayo itauzwa ndani na nje ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nyamagana, Witness Makale amemshukuru naibu waziri huyo kwa kuunga mkono juhudi za kinamama hao.