MABALOZI WAWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

0
152

Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wateule wa nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapo nchini.
 
Hafla ya kupokea hati hizo imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
 
Hati hizo za utambulisho ni kutoka kwa Balozi Mteule wa Nigeria hapa nchini, Hamisu Umar Takalmawa, Balozi Mteule wa India nchini Biyana Srikanta Pradhan na Weibe Jakob De Boer ambaye ni Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini.
 
Wengine ni Madina Diaby Kassamba Ganou ambaye ni  Balozi Mteule wa Burkina Faso hapa nchini mwenye Makazi yake Nairobi, Kenya na Gaussou TourĂ©, Balozi Mteule wa Guinea nchini mwenye Makazi Addis Ababa, Ethiopia.