Gwajima na Silaa waondolewa kwenye kamati

0
350

Wabunge Josephat Gwajima wa jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam na Jerry Silaa wa jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam ambao ni wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, wameondolewa kwenye kamati hiyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo.

Hivi karibuni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai aliamuru wabunge Gwajima na Silaa kufika mbele ya kamati hiyo ili kujibu tuhuma mbalimbali.zinnazowakabili ikiwa ni pamoja na kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Emmanuel Mwakasaka.amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, kamati hiyo ilikuwa na wajumbe 24 wakiwamo Gwajima na Silaa, lakini sasa imebaki na wajumbe 22 baada ya Wabunge hao kuwekwa pembeni.

Gwajima alianza kuhojiwa jana na kamati hiyo ambapo kesho ataendelea kuhojiwa, na Silaa anahojiwa leo.