Mwenge wakabidhiwa Lindi  

0
150

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla leo amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa mkoa wa Lindi, baada ya mwenge huo kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 105 mkoani humo.

Shughuli ya kukabidhi Mwenge huo imefanyika mkoani Lindi, ambapo Makalla amesema mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Dar es Salaam zimekuwa na mafanikio makubwa.

Hata hivyo amesema licha ya mafanikio hayo, miradi mitano kati ya 46 imeshindwa kupitishwa na viongozi wa mbio za Mwenge kutokana na kuwa na changamoto kadhaa.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ameahidi kufuatilia kwa kina miradi hiyo na kuhakikisha changamoto zote zilizojitokeza zinashughulikiwa.

Mwenge wa uhuru ulikabidhiwa mkoani Dar es Salaam tarehe 18 mwezi huu ukitokea mkoa wa Pwani,  na kuhitimisha mbio zake tarehe 22 mwezi huu.