Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuthibitisha shutuma alizotoa dhidhi yake za kupokea hongo ili kupokea chanjo za UVIKO-19.
Dkt. Gwajima ameviagiza vyombo vya dola kumchukulia hatua mara moja endapo atashindwa kuthibitisha hilo.
Waziri ametoa agizo hilo leo akiwa kwenye ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya na lishe pamoja na shughuli za maendeleo ya jamii katika Wilaya ya Butiama mkoa wa Mara.