Basil Mramba afariki dunia

0
295

Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo Jumanne, Agosti 17, 2021 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Rais Benjamin Mkapa ambapo aliiongoza Wizara hiyo mwaka 2001-2005, baadaye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2006 hadi 2008.

Familia ya Mramba imethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa ni wanafamilia wachache wataruhusiwa kufika kutoa pole nyumbani kwa marehemu, Mawenzi Road, Oysterbay Dar es Salaam