Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi amesikitishwa na kitendo cha Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kushindwa kutekeleza ujenzi wa makao Makuu ya Halmashauri hiyo licha ya Serikali kutoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa miezi minne (4) kwa Halmashauri pamoja na Mkandarasi Suma Jkt kuhakikisha jengo linakamilika ndani ya muda huo.
Hapi amesema inasikitisha mpaka sasa kuona hatua za awali za ujenzi huo zikiwa hazijafikia hata asilimia 5 ilihali fedha ya ujenzi huo ilitolewa tangu Mwezi Machi Mwaka huu.
Hapi ameonya tabia ya ubinafsi na kutokuwa na uzalendo kwa baadhi ya Watumishi ambao ndio wamekuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo Mkoani humo.
Mpaka sasa ujenzi wa jengo hilo uko katika hatua za awali ambapo tayari Mkandarasi amechimba mashimo huku kasi ikiwa hairidhishi.