General Tyre kuwa eneo la viwanda

0
135

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuuisha eneo la kiwanda cha General tyre na kuwa mtaa wa viwanda “Industrial park” kutokana na kiwanda hicho kutokidhi mahitaji ya kuendelea kufanya uzalishaji wa matairi kulingana na uhitaji wa soko.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichosimama na kuacha kufanya uzalishaji kwa muda wa zaidi ya miaka 10, kutokana na teknolojia ya uzalishaji wa kiwanda kupitwa na wakati pamoja na matairi yaliyokuwa yamezalishwa kukosa soko ambapo amesema kuwa lengo la kufanya eneo hilo kuwa mtaa wa viwanda ni kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuleta ajira kwa watanzania hasa wananchi wa Arusha.