Rais Kagame achanganywa na kipigo cha Arsenal

0
212

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais wa Rwanda na shabiki wa timu ya Arsernal, Paul Kagame ameonesha kuchukizwa kwake na kipigo cha timu ya Arsernal katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England.

Katika mchezo huo timu ya Arsernal ilipigwa bao 2-0 na timu iliotoka kupanda daraja ya Brentford katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo na kuwashangaza wengi.

Baada ya mchezo huo uliochezwa jana Rais huyo ambaye nchi yake inafadhili chapa ya ‘Visit Rwanda’ kwenye jezi ya timu hiyo aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba timu hiyo haipaswi kukubali kuwa ya kawaida na kuongeza kuwa timu inapaswa kujengwa kwa lengo la kushinda pekee.

“We just must NOT excuse or accept mediocrity.A team has to be built with purpose to win win win”

Ufadhili wa serikali ya Rwanda umekuwa na thamani ya kiasi cha dola za Marekani milioni 42. Ufadhili huo umekuwa ukipingwa na baadhi ya watu kutokana na gharama hizo ikilinganishwa na kipato cha nchi ingawa serikali ya Rwanda imekuwa ikisema ufadhili huo unalipa kupitia utalii.