Maji si tatizo tena Kisarawe

0
141

Wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya Kisarawe mkoani Pwani wamesema shida ya maji hospitali ni hapo imebaki kuwa historia baada ya mradi wa maji Kisarawe kukamilika asilimia 100.

Wakizungumza Hospitalini hapo wamesema awali walilazimika kubeba maji kwenye vidumu kutokea majumbani kwa ajili ya matumizi ya vipimo mbali mbali huku uongozi wa hospitali ikitumia zaidi ya milioni mbili kununua maji kwa mwezi.

Wakazi hao wamesema vyoo vilikuwa havina maji ya kusukuma taka na hivyo walilazimika kubeba maji kutoka majumbani kwa ajili ya wagonjwa wao ama wao wenyewe watumie pale wanapowatembelea ndugu zao wagonjwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Yonah Kabata amesema kabla ya kuanza kwa mradi wa maji Kisarawe hospitali hiyo iligharimika kununua maji kwa shilingi laki sita hadi saba kwa wiki kwaajili ya matumizi ya wagonjwa huku wakilazimika kutoa huduma hadi saa sita mchana pekee.

Kukamilika kwa mradi wa maji Kisarawe kumefanikisha kupunguza gharama ya ununuzi wa maji hadi shilingi laki sita kwa mwezi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi amekagua mradi huo na kuridhishwa na maendeleo yake na kuwataka wakazi wa Mkuranga kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya miradi ya maji.