Wawekezaji waongezeka Tanzania

0
939

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili jumla ya miradi 235 katika kipindi cha mwezi Juni 2020 mpaka Julai mwaka huu ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 3.3, sawa na ongezeko la asilimia 8 ya miradi.

Akitoa taarifa hiyo mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Maduhu Kazi amesema kati ya miradi iliyosajiliwa miradi 66 ambayo asilimia 28 ni ya Watanzania, na miradi 65 iliyosajiliwa ni miradi ya ubia kati ya watanzania na wageni huku iliyobaki ikiwa ni miradi ya kigeni.

Aidha, Maduhu ameongeza kuwa uboreshwaji mkubwa umefanyika katika mifumo ambayo hutumiwa na idara ya uhamiaji na idara ya kazi ili kutoa vibali haraka kwa wawekezaji katika kituo cha pamoja.