Waitara awataka watendaji kigoma kushirikiana

0
198

Naibu waziri ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara amezitaka taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha utendaji kazi.

Akizungumza na watumishi wa taasisi hizo mkoani Kigoma naibu Waziri Waitara pamoja na mambo mengine amesema ushirikiano katika kazi ndiyo silaha ya mafanikio.

Aidha amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kusisitiza kutowavumilia watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma.

Katika kikao hicho pia naibu waziri Waitara amesisitiza nia ya serikali kuendelea kufungua mkoa wa Kigoma katika sekta ya miundombinu hususani barabara reli,usafiri wa anga na majini.