Aweso aunguruma Geita

Miradi ya Maji

0
157

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amevunja kamati ya maji ya kijiji cha Mharamba iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Geita baada ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazolipwa na wananchi kupatiwa huduma ya maji.

Aweso amevunja kamati hiyo na kuagiza RUWASA kuboresha vituo 3 vilivyobakia vianze kutoa maji ndani ya siku 14.

Aidha Aweso amezitaka kamati za vijijini kuweka utaratibu mzuri wa matumizi na ukusanyaji wa fedha kutokana na uwepo wa baadhi ya kamati kutafuna fedha zinazokusanywa kwenye miradi ya serikali.