Taliban yaichukua Ikulu, Rais akimbia.

0
239

Wakati zaidi ya nchi 60 zikiomba kuondoka kwa amani kwa wageni nchini Afghanistan, kundi la Taliban limetangaza vita kuisha baada ya kuingia mji Mkuu Kabul na Rais Ashraf Ghani kukimbia nchi.

Mitaa ya Kabul imekuwa kimya siku ya leo, lakini kulikuwa na hali ya vurugu katika uwanja wa ndege wa Kabul kufuatia mamia ya wakazi kutaka kukimbia nchi hiyo.

Marekani na nchi nyingine za magharibi pia zimekuwa zikipambana kuwaondoa wanadiplomasia wao waliomo nchini humo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litajadili hali nchini Afghanistan baadaye leo.