DC Mbeya apiga ‘stop’ matangazo ya misiba

0
181

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Dkt. Rashid Chuachua amepiga marufuku magari ya matangazo ya misiba jijini humo, baada ya kuchukua miili ya watu waliofariki kwenye hospitali za Serikali, kwa madai kuwa yamekuwa yakileta hataruki kwa wananchi na kujenga hofu.

Chuachua ameagiza kamati ya ulinzi na usalama kufanya doria na kuwachukulia hatua wamiliki wa magari hayo watakaobainika.

“Kumekuwa na tabia ya familia za watu wanaopoteza maisha kukodi magari ya matangazo na kuanza kutangaza maeneoa mbalimbali ya jiji na kutaja majina ya wapendwa wao sasa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa nimepiga marufuku rasmi leo Agosti 10 2021,” amesema Chuachua.

Dkt. Chuachua amesema agizo hilo lianze mara moja na ndugu yoyote anayefikwa na msiba wawasiliane kama familia kufanya taratibu za mazishi na kuhusu suala la matangazo kutoka hosptali mpaka kwenye maziko marufuku, pia mikusanyiko ya watu hairuhusiwi kwa kipindi hiki cha kuibuka kwa covid 19 awamu ya tatu.

Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya ,Dourmohamed Issa amesema kuwa uamuzi wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ambaye ni Mkuu wa Wilaya, ni sahihi kwani kumekuwa na taharuki kubwa kwa jamiii pindi magari ya matangazo na inayobeba miili ya waliopoteza maisha ikipita barabara kuu.