Hapi aagiza taarifa za mapato na matumizi kutolewa

0
146

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amewataka watendaji wa vijiji na kata kutoa taarifa za mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Hapi amesema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kata ya Machochwe wilayani Serengeti juu ya kutoshirikishwa katika hatua mbalimbali za miradi ikiwemo usiri wa matumizi ya fedha katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Machochwe.

Amewataka watendaji na viongozi wa Serikali kuacha tabia hiyo mara moja kwani wananchi ndio wenye serikali hivyo ni lazima washirikishwe katika hatua zote kwa uwazi.

Hapi ameanza ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali katika halmashauri zote za mkoa wa Mara.