Utafiti: Chanjo ya J&J madhubuti kuzuia vifo vya UVIKO-19

0
284

Tafiti iliyofanywa kupima uwezo wa chanjo ya Johnson & Johnson (J&J) imeonesha uwezo mkubwa wa chanjo hiyo kupambana na wimbi la tatu la UVIKO-19 (Delta).

Tafiti hiyo iliyofanyika Afrika Kusini imeonesha kuwa J&J ina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya wimbi la tatu la UVIKO-19 kwa 71% na kupunguza uwezekano wa kulazwa huku ikitoa 91% hadi 96.2% dhidi ya vifo vitokanavyo na Korona.

Chanjo ya J&J iliingia nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Julai, na kuzinduliwa Julai 28 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wananchi wanaendelea kujitokeza katika vituo mbalimbali katika mikoa yote nchini kupatiwa chanjo hiyo ili kujikinga na athari za maambukizi virusi vya korona.