Wananchi Kilimanjaro wasisitiza kuwa chanjo ni salama

0
165

Na Sauda Shimbo,

KILIMANJARO

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mtanda ameongoza wananchi wa mkoa huo kupata chanjo ya UVIKO-19 Agosti 3, 2021.

Akizungumza wakati akizindua zoezi la kuanza kwa chanjo hiyo kimkoa katika Kituo cha Afya Majengo, Manispaa ya Moshi, Mtanda amesema tayari mkoa umepokea chanjo 10,000 kati ya 60,000 ambazo zitatolewa katika wilaya zote za mkoa huo.

Amesema wananchi wote wataokaojitokeza kupata chanjo hiyo watachanjwa na hakuna atayekosa kwani zipo za kutosha.

Pia amewataka watumishi wa afya kuwapa kipaumbele wazee katika kupatiwa chanjo na atakayekiuka agizo hilo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kupatiwa chanjo hiyo wamesema hawajapata madhara yoyote na kwamba ni vyema wananchi wakaacha kusikiliza maneno ya mitaani kwamba chanjo hiyo haina madhara.