Bashe: Tutaanza kuuza Parachichi zetu Afrika Kusini

0
153

Naibu waziri wa Kilimo Hussein Bashe amsema kuanzia msimu huu Mazao ya Parachichi yanayozalishwa hapa nchini yataanza kuuzwa katika soko la Afrika Kusini.

Bashe amesema, taratibu zinaendelea vizuri na kwamba msimu huu, mazao hayo yataanza kuuzwa nchini humo licha kwamba hapo awali yalizuiliwa kuuzwa katika soko hilo.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Mbeya, Naibu waziri Bashe amesema, hapo awali Parachichi ilizuiliwa kuingizwa katika soko la Afrika ya Kusini lakini mazungumzo yanaendelea ili mazao hayo yaingie katika soko hilo.

Kuhusiana na zao la Chai, Bashe amsema msimu huu Chai ya Tanzania haitauzwa tena katika soko la Kenya, bali kutafanyika mnada mkubwa katika Bandari ya Dar es salaam na wanunuzi watanunua katika mnada huo.

Bashe ameongeza kuwa huo utakuwa mnada mkubwa zaidi wa zao la Chai barani Afrika ukitanguliwa na Mnada wa Malawi na ule wa Mombasa Kenya.