Waziri Mkuu aagiza kurejeshwa safari za MV Mbeya II

0
135

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kusimamia kwa karibu kuanza kwa safari za meli ya MV Mbeya II zilizosimama kwa muda mrefu na kusababisha adha ya usafiri.

Ametoa agizo hilo Mara baada ya kutembelea Bandari ya Itungi iliyopo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya ambapo amekagua maendeleo ya matengenezo ya meli ya MV Mbeya II inayokarabatiwa na kampuni ya Songoro Marine baada kupata hitilafu za kiufundi miezi mitatu iliyopita.

Majaliwa pia amewaagiza TPA kuhakikisha wanafanya mazungumzo ya kibiashara kati ya Malawi na Tanzania ili kuruhusu shehena za mizigo yakiwemo makaa ya mawe kusafirishwa nchini humo.

Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kyela kuhakikisha anakaa na uongozi wa bandari mara kwa mara ili kujenga mahusiano na vijiji vinavyozunguka Ziwa Nyasa.