Mbunge wa CCM ajiuzulu

0
164

Mbunge wa Jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki amejiuzulu ubunge kuanzia leo Agosti 2, 2021 kutokana na sababu za kifamilia.

Amefikia uamuzi huo kutokana na “changamoto za kifamilia jambo ambalo chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM” imeeleza barua hiyo iliyoandikwa na Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Faki aliyekuwa akisubiri kuapishwa alichaguliwa Julai 18, 2021 katika uchaguzi mdogo kufuatia aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Khatib Said Haji kufariki dunia.