RAIS : WATANZANIA TUMIENI FURSA ZILIZOPO

0
213

Rais Samia Suluhu Hassan, amewasihi watanzania kutumia fursa ya miundombinu ili kuwa na maendeleo ya kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa hafla ya mapokezi ya ndege mpya aina ya Bombardier Dash 8-400, iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Pia Rais Samia amesema Tanzania inatarajia kununua ndege ya kusafirisha mizigo ili kukuza uchumi wa nchi na kuwahimiza watanzania kujipanga vyema ili kunufaika na fursa za mindombinu inayojengwa nchini.

Vilevile Rais Samia amegusia swala la utalii “Ili nchi iweze kuvutia watu wengi watalii, lazima iwe na shirika la ndege lililo imara, tumefanya upanuzi wa viwanja vyetu lakini kazi yakuendelea kupanua viwanja inaendelea,”-amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia Rais amewasisitiza ATCL kutunza ndege zinazonunuliwa na kuepuka hujuma bali wajikite katika kuboresha huduma za usafiri nchini.