UVIKO19 kupimwa kwa dakika 39

0
288

Katika Hospitali ya Kijeshi na Magonjwa ya Mlipuko iliyozindualiwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan, wananchi wataweza kupima magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na UVIKO-19 ambapo kuna mashine inayoweza kutoa majibu ndani ya dakika 39 na nyingine dakika 44.

Mbali na hilo wananchi wataweza kupima magonjwa kama vile UKIMWI, Ebola, magonjwa ya moyo na figo.

Ujenzi wa hospitali hiyo ya aina yake ulianza Aprili mwaka 2018, ambapo upanuzi zaidi ulifanyika tofauti na mpango wa awali kutokana na mlipuko wa janga la Korona, ili kuiwezesha nchi kukabiliana na magonjwa kama hayo.

Awali kituo hiki hakikupangwa kuwa cha kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, bali kilikusudiwa kuwa hospitali kwa ajili ya wanajeshi wanaokwenda kuhudumu katika ulinzi wa amani kwenye nchi nyingine.